Friday, September 13, 2013

Askali wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania katika mpaka wa Tunduma uliopo kati ya Tanzania na Zambia, wamefanikiwa kuzima machafuko yaliyokuwa yameanza kati ya wasafirishaji wa Tanzania na Zambia. Sakata hilo lilitokea juzi kuanzia majira ya saa 2 asubuhi na kumalizika majira ya saa 9 alasiri ambapo wasafirishaji wa upande wa Tanzania walikuwa wakinyang’anya funguo za magari ya raia wa Zambia waliokuwa wakivuka mpakani hapo kwa kile walichodai kuwa walichoshwa na manyanyaso. Walisema kuwa raia wa Zambia wamekuwa wakiwapiga wasafirishaji kutoka upande wa Tanzania hasa wanaosafirisha kwa kutumia Bajaji na pikipiki maarufu kama Bodaboda wanapovuka kwenda eneo la Nakonde kupeleka abiria jambo ambalo walilipeleka polisi mara kadhaa lakini walikuwa wakipuuzwa. Wasafirishaji hao walisema kuwa tabia hiyo ya wasafirishaji wa upande wa Zambia imedumu kwa takribani muda wa miezi miwili sasa hivyo nao waliamua kujichukulia hatua mikononi ili Serikali za pande zote mbili zichukue hatua kudhibiti maonezi wanayotendewa. Baada ya hali hiyo kuwa tete, Askari wa Jeshi la polisi katika kituo cha polisi kilichopo Tunduma waliamua kujitokeza na kuwaomba wasafirishaji hao kutoa kero zao na kile kilichosababisha waanze kujichukulia hatua ili kuwadhibiti raia wa Zambia kutoingia na usafiri wao upande wa Tunduma ambapo wasafirishaji hao walitii ombi hilo. Askari Polisi hao wenye vyeo mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa kituo hicho Aly Wendo waliwasihi wasafirishaji hao kuacha kufanya hivyo kwa kile walichodai kuwa malalamiko yao yalikuwa ya Msingi lakini wakawaonya kuwa ni muhimu wakaheshimu sheria za nchi zingine. ‘’Tunawashukuru kwa uelewa wenu na kutoa malalamiko bila kuficha na sisi kwasababu tunajua maana ya ujirani mwema na askari wa upande wa pili wanauelewa mzuri hivyo mimi ninaenda kule upande wa pili kuwaeleza wenzangu kuwa kuna jambo hilo hivyo atakayepigwa kuanzia sasa aje kwangu tunavuka nae na kuwakamata wale watakao husika’’ alisema Wendo. Kwa upande wake Inspector Chaburuma na askari wengine ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja waliwafafanulia wasafirishaji hao kuwa sheria za nchi ya Zambia hazitambui usafiri wa Bodaboda na bajaji hivyo ni muhimu wakaheshimu suala hilo licha ya kuwepo mazoea ya ujirani mwema. Kwa upande wao wasafirishaji hao zaidi ya 100 waliokuwa wametoka eneo la mpaka huo walipokuwa wamezingira na kisha kuelekea katika kituo cha polisi baada ya kuombwa na askari polisi wa Tunduma waliwahakikishia askari hao kuwa wamekubaliana na ushauri huo na hasa kutokana na Mkuu huyo wa kituo kuonesha utu wa kufuatilia upande wa pili ili kumalizwa kwa mgogoro unaoweza ukuathiri uchumi wa watu wanaotegemea mpaka huo. Msafirishaji Hamad Omary alisema kuwa kutokana na kueleweshwa na askari hao msafirishaji yeyote ambaye atakiuka makubaliano hayo wenzake hawatahusika na

Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya Cheju Zanzibar,Joseph Mwangamba amemwagiwa tindikali na kujeruhiwa usoni na kifuani source..East Africa Radio.

YANGA YAITEKA MBEYA

Kikosi cha timu ya Young Africans kimefanya mazoezi yake ya kwanza mkoani Mbeya katika viwanja vya shule ya sekondari Iyunga jioni ya leo kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Mbeya City katika dimba la uwanja wa Sokoine. Msafara mkubwa ulijitokeza kukipokea kikosi cha Yanga jana jioni kuanzia maeneo ya kituo cha mafuta cha TAZAMA na kuongozana na mashabiki, wapenzi na wanachama waliojitokeza kuipokea timu mpaka eneo la soweto ilipofikia. Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara Young Africans wamefanya mazoezi leo kufuatia jana kuwa safarini kutoka jijini Dar es salaam ambapo timu iliwasili majina ya saa 12:30 na kufikia katika hoteli ya Mbeya Paradise Inn iliyopo maeneo ya soweto jijini Mbeya. Wachezaji wamefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts huku wapenzi washabiki na wanachama wakijoitokeza kwa wingi kukishuhudia kikosi cha watoto wa jangwani ambao wameliteka jiji la Mbeya tangu kufika kwake. Mara baada ya mazoezi ya leo kocha ameseam kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi na anaamin timu yake itapata ushindi na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu msimu huu. Aidha viongozi wa Yanga, benchi la ufundi na wachezaji wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapaa kutoka kwa wenyeji Tawi la Yanga mkoani Mbeya ambao wamejitolea muda wao wote kuwa na timu bega kwa bega katika maandaliz ya mchezo huo wa jumamosi. Kesho majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki timu itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine tayari kabisa kwa kuikabili timu ya Mbeya City siku ya jumamosi. Last Updated ( Thursday, 12 September 2013 18:52 )

picture