Friday, September 13, 2013
Askali wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania katika
mpaka wa Tunduma uliopo kati ya Tanzania na
Zambia, wamefanikiwa kuzima machafuko
yaliyokuwa yameanza kati ya wasafirishaji wa
Tanzania na Zambia.
Sakata hilo lilitokea juzi kuanzia majira ya saa
2 asubuhi na kumalizika majira ya saa 9 alasiri
ambapo wasafirishaji wa upande wa Tanzania
walikuwa wakinyang’anya funguo za magari ya
raia wa Zambia waliokuwa wakivuka mpakani
hapo kwa kile walichodai kuwa walichoshwa na
manyanyaso.
Walisema kuwa raia wa Zambia wamekuwa
wakiwapiga wasafirishaji kutoka upande wa
Tanzania hasa wanaosafirisha kwa kutumia
Bajaji na pikipiki maarufu kama Bodaboda
wanapovuka kwenda eneo la Nakonde kupeleka
abiria jambo ambalo walilipeleka polisi mara
kadhaa lakini walikuwa wakipuuzwa.
Wasafirishaji hao walisema kuwa tabia hiyo ya
wasafirishaji wa upande wa Zambia imedumu
kwa takribani muda wa miezi miwili sasa hivyo
nao waliamua kujichukulia hatua mikononi ili
Serikali za pande zote mbili zichukue hatua
kudhibiti maonezi wanayotendewa.
Baada ya hali hiyo kuwa tete, Askari wa Jeshi la
polisi katika kituo cha polisi kilichopo Tunduma
waliamua kujitokeza na kuwaomba wasafirishaji
hao kutoa kero zao na kile kilichosababisha
waanze kujichukulia hatua ili kuwadhibiti raia
wa Zambia kutoingia na usafiri wao upande wa
Tunduma ambapo wasafirishaji hao walitii ombi
hilo.
Askari Polisi hao wenye vyeo mbalimbali
wakiongozwa na mkuu wa kituo hicho Aly
Wendo waliwasihi wasafirishaji hao kuacha
kufanya hivyo kwa kile walichodai kuwa
malalamiko yao yalikuwa ya Msingi lakini
wakawaonya kuwa ni muhimu wakaheshimu
sheria za nchi zingine.
‘’Tunawashukuru kwa uelewa wenu na kutoa
malalamiko bila kuficha na sisi kwasababu
tunajua maana ya ujirani mwema na askari wa
upande wa pili wanauelewa mzuri hivyo mimi
ninaenda kule upande wa pili kuwaeleza
wenzangu kuwa kuna jambo hilo hivyo
atakayepigwa kuanzia sasa aje kwangu tunavuka
nae na kuwakamata wale watakao husika’’
alisema Wendo.
Kwa upande wake Inspector Chaburuma na
askari wengine ambao majina yao hayakuweza
kupatikana mara moja waliwafafanulia
wasafirishaji hao kuwa sheria za nchi ya
Zambia hazitambui usafiri wa Bodaboda na
bajaji hivyo ni muhimu wakaheshimu suala hilo
licha ya kuwepo mazoea ya ujirani mwema.
Kwa upande wao wasafirishaji hao zaidi ya 100
waliokuwa wametoka eneo la mpaka huo
walipokuwa wamezingira na kisha kuelekea
katika kituo cha polisi baada ya kuombwa na
askari polisi wa Tunduma waliwahakikishia
askari hao kuwa wamekubaliana na ushauri huo
na hasa kutokana na Mkuu huyo wa kituo
kuonesha utu wa kufuatilia upande wa pili ili
kumalizwa kwa mgogoro unaoweza ukuathiri
uchumi wa watu wanaotegemea mpaka huo.
Msafirishaji Hamad Omary alisema kuwa
kutokana na kueleweshwa na askari hao
msafirishaji yeyote ambaye atakiuka
makubaliano hayo wenzake hawatahusika na
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment