Monday, September 9, 2013
Damu ya Yesu yamnasa Mchawi IJUMAA KUU
Mbeya ni kijana Jofrey Japhet.
Na, Ezekiel Kamanga, Mbeya.
KIJANA Jofrey Japhet(18), mkazi wa Kijiji cha
Nanyala wilayani Mbozi mkoani Mbeya
amenaswa na kile kilichoelezwa kuwa ni nguvu
za Mungu siku ya Ijumaa Kuu jana.
Tukio hilo limetokea leo eneo la Nzovwe Jijini
Mbeya majira ya saa kumi alfajiri katika
viwanja vya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli
Tanzania (KKKT) ambapo mkutano wa Injili
ulikuwa ukiendelea.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi
aliyefika mapema eneo la tukio, kijana huyo
alisema kuwa alikuwa pamoja na mjomba wake
aliyemtaja kwa jina la Edwin Mwakaswila
ambaye alimtuma kijana huyo kumchukua binti
ambaye alitakiwa waongozane kwenye safari
kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa.
��Nilikuwa na Mjomba wangu anayeitwa
Edwin Mwakaswila tukielekea Sumbawanga kwa
ajili ya kwenda kuongezewa cheo cha nguvu za
giza(uchawi) ndipo tulipofika hapa akaniambia
niingie kanisani kumchukua Ester Mwashilindi
ili tuende nae ndipo nikazidiwa na kushindwa
kuondoka ndani ya kanisa walipokuwa
wamelala waumini wengi�� alisema kijana
huyo.
Aidha aliweka wazi kuwa baada ya kuingia
ndani ya kanisa hilo kwa ajili ya kumchukua
Ester akakosea njia na kumwamusha Enock
Mwandagane ambaye alishituka na kumkuta
akiwa utupu hali ambayo ikamaliza nguvu za
kichawi alizokuwa nazo.
Baada ya hapo Mwandagane aliwaamusha
waumini wenzake na kuanza kumfanyia
maombi kijana huyo huku baadhi ya wasamaria
waiwemo wanawake wakimsitiri kwa Kanga
utupu wake.
Kijana huyo alimtaja Mlafwaya Mwanguluma
ambaye anaishi ziwa Rukwa kuwa ndiye mkuu
wao wa mambo ya giza ambako ndiko
walitarajia kwenda kuongezewa vyeo hivyo vya
kichawi ili kijana huyo awe mkuu wa
washirikina katika makaburi Jijini Mbeya.
Kwa upande wake kiongozi wa huduma ya
Maisha mapya ndani ya Kristo (New Life Crist)
Amon Mwangosi alisema kijana huyo amekutwa
mara nyingi katika mikutano mbalimbali ya
Injili akikusudia kuvuruga huduma hiyo ya
Mungu hivyo alichukua maamuzi ya kumpeleka
katika kituo kidogo cha Polisi cha Nzovwe ili
kumwepusha na gadhabu za wananchi wenye
hasira kali.
Kijana huyo baada ya kufikishwa katika kituo
hicho cha polisi aliondolewa na kupelekwa
katika kituo kikuu cha polisi kwa gari yenye
namba za usajiri T502 AGD.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment